Image
Image

TFF Yaunda Kamati Ya Taifa Stars kuelekea mchezo wake na Algeria.


Katika kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa “Kamati ya Taifa Stars” ambayo majukumu yake yatakua:
(i) Kuimarisha huduma kwa wachezaji,
(ii) Uhamasishaji na Masoko,
(iii) Kuhamasisha wachezaji,
(iv) Kuandaa na kusimamia mkakati wa Ushindi.
Kamati hii itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
Aidha Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.
Wadau wa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika kamati hiyo wanaombwa waitikie wito huo.
          Stars Vs Algeria Kupigwa Novemba 14 Taifa Dar es Salaam.
Hata hivyo Mchezo wa hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Algeria (The Fox Desert) utafanyika tarehe 14 Novemba, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Taifa Stars itacheza mchezo huo dhidi ya Mbweha hao wa Jangwani siku ya Jumamosi Novemba 14, na mchezo wa marudiano kuchezwa siku tatu baadae Algeria 17 Novemba, 2015.
Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment