Kiongozi wa China Rais XI JINPING anatarajia kutia saini mkataba wa kuchangia kile kinachoonekana kuwa mtambo mkubwa wa kwanza wa nishati ya nyuklia kuwahi kujengwa na Uingereza.
Mkataba huo ni sehemu ya ziara ya siku nne ya Bwana XI huko Uingereza na mtambo huo wa nishati ya nyuklia ambao China itagharimia asilimia 30 ya ujenzi wake unatarajiwa kufunguliwa mwaka 2025
Kiongozi huyo wa China baadaye leo anatarajia kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bwana DAVID CAMERON katika siku ya pili ya ziara yake ambayo mikataba ya pauni bilioni 30 sawa na dola bilioni 50 inatarajiwa kutiwa saini kati ya nchi hizo mbili.
Wakati wa dhifa ya siku yake ya kwanza ya ziara hiyo Malkia ELIZABETH wa Uingereza alielezea uhusiano wa nchi zao mbili kama ushirika wa kimataifa na kutaja ziara ya Rais XI kama ya kufana.
0 comments:
Post a Comment