Image
Image

Ukubwa wa theluji waanza kupungua katika Mlima Kilimanjaro.

Tafiti za sayansi zinazoendelea kufanywa na wanasayansi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,zinaonesha kuendelea kupungua kwa kasi,ukubwa wa theluji katika Mlima Kilimanjaro.
Tafiti zinaonesha  sasa umebaki na ukubwa wa karibu Kilomita mbili tu za mraba ikilinganishwa na Kilomita 20 za mraba za theluji zilizokuwepo miaka ya nyuma na enzi za ukoloni.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, ERASTUS LUFUNGULO amesema tafiti hizo zilizoanza kufanyika miaka zaidi ya 100 iliyopita haziwezi kupuuzwa na kwamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya kimataifa,  juhudi zinaendelea kufanywa ili kunusuru kutoweka kwa theluji ya mlima kilimanjaro, mlima mrefu kuliko yote Barani Afrika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania,  ALAN KIJAZI akizungungumzia kuhusu hali hiyo amesema mlima huo una mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii na taifa na juhudi zinafanywa kubaini ukubwa wa tatizo ili kuchukua hatua sahihi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment