Watanzania zaidi ya Elfu-Moja na 660 wenye asili ya nchi za Rwanda na Burundi wenye uraia wa kuandikishwa wanaoishi Mkoani Kagera huenda wasishiriki kwenye zoezi la upigaji kura.
Hiyo inatokana na zoezi linaloendelea hivi sasa linalofanywa na Idara ya Uhamiaji hapa nchini la kuhakiki uhalali vibali vyao vya kuishi nchini lililoanza tangu mwaka 2006 iwapo litadumu hadi siku ya upigaji wa kura.
Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoani Kagera kwa maofisa wa idara hiyo, juu ya elimu ya uraia na haki ya mpiga kura, Naibu Kamishiina wa Uhamiaji, JUSTINE KEWISA amesema idara hiyo ilifikia uamuzi wa kuhakiki vibali hivyo, baada ya kubaini udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya raia hao wa kughushi vibali hivyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, JOHN MONGELLA amewataka maofisa uhamiaji katika kipindi hiki cha uchaguzi wasimamie sheria na wasikubali kuyumbishwa na wanasiasa.
0 comments:
Post a Comment