Image
Image

Netanyahu, ashindwa katika vita vya kichokozi huko Quds Tukufu.

Katika mwendelezo wa machafuko huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu Wizara ya Afya ya Palestina imeripoti idadi ya watu 46 kuuawa shahidi katika Intifadha mpya na wengine 5452 kujeruhiwa. 
Kuendelea kimya cha Umoja wa Mataifa kuhusiana na kadhia hiyo, kumeufanya utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza jinai zake katika eneo la Quds. Habari zinaarifu kuwa hapo juzi kundi la walowezi wa Kizayuni walivamia msikiti wa al-Aqsa, chini ya ulinzi mkali wa askari wa usalama wa utawala wa Kizayuni kupitia mlango wa 'Babul-Maghaaribah' sanjari na kuweka askari 300 wa Kizayuni katika eneo hilo. Hatua hiyo iliyochukuliwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri la Utawala wa Kizayuni, ina lengo la kushadidisha mzingiro wa kiusalama katika eneo hilo. Israel ina matumaini kwamba, kuweka askari hao 300 katika eneo hilo kutasaidia kuimarisha usalama kwa Mayahudi wanaoishi eneo la Quds kutokana na hasira ya Wapalestina. Tangu ulipoanza mgogoro wa sasa ulioibuliwa na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel, mabasi ya abiria yamekuwa yakionekana kwa wingi katika eneo hilo la Quds kutokana na woga wa Wazayuni. Baada ya wiki mbili tangu kutokea machafuko hayo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, hususan eneo la Quds, kumeendelea kushuhudiwa jinai mbalimbali za askari na walowezi wa Kiyahudi wenye misimamo mikali dhidi ya raia wa Palestina. Hivi karibuni Benjamin Netanyahu alisikika akiwahamasisha Mayahudi wenye misimamo ya kufurutu ada wawapige Wapalestina hadi kufa. Baada ya matamshi hayo ya kichochezi, haukupita muda kabla ya karibu maeneo yote ya Palestina kuanza kushuhudia machafuko. Takwimu za hivi karibuni zilizofanywa huko Israel, zinaonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa uungaji mkono wa Wazayuni kwa Netanyahu, kutokana na kuendelea kwa Intifadha ya Quds na machafuko ya hivi karibuni katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, iliyochapishwa na gazeti la lugha ya Kiebrania, theluthi mbili ya wakazi wa Tel-Aviv, mji mkuu wa Israel, wanaunga mkono mpango kikamilifu kuondoka askari na walowezi wa Kizayuni kutoka katika eneo la mashariki mwa Quds. Weledi wa mambo wanaamini kwamba, hatua ya Netanyahu ya kupuuza malalamiko ya ndani na pia migogoro ya kiuchumi ya Israel, ni sababu ya kuongezeka makundi ya vijana wenye misimamo mikali katika jamii ya Kizayuni, suala ambalo limeendana na kupanuka machafuko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Katika mazingira hayo, Quds na maeneo mengine matukufu, yamekuwa yakilengwa kila mara kiasi cha kulifanya baraza la mawaziri lenye misimamo ya kufurutu ada la Netanyahu kupasicha mswada wenye ncha mbili, yaani kuwaua kwa umati raia madhlum wa Palestina na kuwaondoa katika mji huo na wakati huo huo kuendelea kuudhibiti mji huo mtakatifu. Kujiri Intifadha katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu mwaka 1987, ni mambo yaliyokwamisha njama za kupenda kujitanua za watawala wa Kizayuni. Hakuna shaka kuwa, hatua ya Benjamin Netanyahu ya kuwachochea walowezi wa Kiyahudi wenye misimamo mikali kulikotanguliwa na kutangazwa kusimamishwa mazungumzo ya pande mbili na Mamlaka ya Ndani ya Palestina, sanjari na uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqsa ambacho ni kibla cha kwanza cha Waislamu, kulikuwa na lengo la kumfanya waziri mkuu huyo aweze kufikia ushindi wa mwisho. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa Wapalestina, Netanyahu atashindwa tu kama alivyoshindwa mtangulizi wake Ariel Sharon kufikia malengo yake hapo mwaka 2000, baada ya kuingia katika msikiti huo wa al-
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment