Vyombo vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimemtia mbaroni kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Palestina Hamas.
Askari wa utawala huo ghasibu walivamia makazi ya Hassan Yousef katika mji wa Beitunia, kusini magharibi mwa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Utawala huo haramu ulikuwa umemkamata na kumzuilia pasina kumpandisha kizimbani kiongozi huyo wa Hamas mwezi Juni mwaka huu, na baadaye kumuachia huru.
Huku hayo yakijiri, vikosi hivyo vinawashikilia Wapalestina 35, waliowakamata usiku wa kuamkia leo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Jeshi la Israel limewaua shahidi Wapalestina wapatao 46 tangu kuanza Intifadha ya 3 mapema mwezi huu wa Oktoba.
0 comments:
Post a Comment