Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Mkoani Kagera wameitupia lawama Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushindwa kusambaza mapema elimu juu ya mambo yaliyopaswa kuzingatiwa na wananchi na viongozi wa vyama vya siasa katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua ya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi hadi wakati wa zoezi la upigaji kura.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakati wa semina maalumu iliyoandaliwa tume kwa viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo, iliyokuwa na lengo la kujadili matatizo mbalimbali yanayohusiana na mwenendo mzima wa uchaguzi wamesema, ukosefu wa elimu ya kutosha miongoni mwa wananchi juu ya masuala yanayohusu uchaguzi kuwa ndio sababu inayoigharimu tume ya hiyo katika kutoa maelekezo ambayo wakati mwingine yamekuwa yakipingwa.
Katibu wa chama cha NCCR-Mageuzi wa Mkoa wa Kagera, PETERSON MSHEMELA ameeleza kuwa chama chake kitalinda kura kwa nguvu zote na kitaendelea kuwahamasisha wananchi wabaki kwenye vituo baada ya kupiga kura.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi, Wilaya ya Bukoba Mjini, GEORGE SANKA amewahimiza wapigakura waondoke nyumbani baada ya kupiga kura wakasubuiri matokeo.
0 comments:
Post a Comment