Bunge la Libya
linalotambulika kimataifa limeamua kuongeza muda wa uongozi hadi tarehe 20
Oktoba.
Msemaji wa bunge hilo
aliarifu kuchukuliwa kwa uamuzi huo na wanachama wanaotarajiwa kuikabidhi
mamlaka kwa bodi mpya ya uongozi itakayochaguliwa baada ya uchaguzi.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba wanachama wa bunge la Libya pia walichukuwa hatua hiyo
ili kuepuka shinikizo wakati wa mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na UN.
Nchi ya Libya imekuwa ikikumbwa na mizozo ya kisiasa tangu
mwaka 2011 baada ya kupinduliwa kwa Muammar Gaddafi.
Kwa sasa serikali ya Libya inaongozwa na serikali mbili
pinzani zilizojigawa na kufanya mazungumzo ya amani chini usimamizi wa UN.
0 comments:
Post a Comment