Tangu siku ya Jumamosi, vijana Wakipalestina
wamekuwa wakikabiliana na askari wa Israel. Viajana wa Kipalestina wamekua
wakitumia mawe kwa kukabiliana na vikosi vya usalama vya Israel.
Vita hivi vya Intifada vinakumbusha matukio ya mwaka
1987 na 2000, na wakati huu vinayofanyika katika maeneo ya Magharibi na pia
katika baadhi vitongoji vya Jerusalem ya Mashariki.
Lakini hali iliripotiwa kuwa mbaya zaidi Jumatatu
wiki hii katika Ukingo wa magharibi wa mto Jordan, ambapo kijana mdogo wa
kipalastina ameuliwa kufuatia mapigano yaliyolihusisha jeshi la Israel na kundi
la wapiganaji wa Hamas karibu na mji wa Bethlehem, vyanzo vya hospitali za
Palastina vimebainisha.
Machafuko zaidi yamekuwa yakiripotiwa katika siku za
hivi karibuni katika mji wa Jerusalem na katika Ukingo wa magharibi kutokana na
hali tete iliyoko katika eneo la Harami Sharif kunakopatikana msikiti Mtakatifu
wa Al Aqsa.
Jumatatu wiki hii Waziri mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu ameahidi kupitisha hatua kali kukabailiana na Wapalastina wanaohusika
na mashambulio dhidi ya Waisrael.
Wakati huo huo Israel imesema maafisa wake wa
usalama wamewakamata washukiwa watano wa kundi la Hamas kwa tuhma za kuwauawa
raia wake wawili katika eneo la Ukingo wa Magharibi.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema serikali yake
itamchukulia hatua kali yeyeote atakayepatikana kutekleza mauaji hayo.
Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa katika
eneo hilo la Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem kati ya washukiwa
wa Hamas na wanajeshi wa Israel.
Inadaiwa kuwa Hamas walitekeleza mauaji hayo baada
ya wanajeshi wa Israel kumpiga na kumuua kijana mmoja wa Palestina.
Jumuiya ya Kimataifa imeendelea kutoa wito kwa
usitishwaji wa makabiliano haya kwa hifu yanaweza kuendelea kwa muda mrefu na
kusabisha maafa zaidi.
Rais wa Palestina Mahmud Abbas baada ya kukutana na
wakuu wake wa usalama mjini Ramallah ameishtumu Israel kwa machafuko
yanayoendelea kushuhudiwa huku Netanyahu naye akishinikizwa kutumia nguvu zaiid
dhidi ya kundi la Hamas.
0 comments:
Post a Comment