Image
Image

Waziri wa zamani wa mafuta Nigeria akamatwa UK.

Serikali ya Nigeria imetangaza kutiwa mbaroni waziri wake wa zamani wa mafuta mjini London, Uingereza. 
Taarifa iliyotolewa na Garba Shehu, msemaji wa Ikulu ya rais nchini Nigeria imesema kuwa, Diezani Alison-Madueke, waziri wa zamani wa mafuta wa nchi hiyo ametiwa mbaroni jijini London kwa tuhuma za kusafisha fedha na pia kuhusika na ubadhirifu wa mali ya umma nchini mwake. 
Garba Shehu amesema kuwa, waziri huyo wa zamani ametiwa mbaroni kupitia ushirikiano uliopo baina ya idara ya usalama ya Nigeria na taasisi za usalama za nchini Uingereza. Tayari familia ya Diezani Alison-Madueke imethibitisha habari ya kutiwa mbaroni shakhsia huyo. Diezani mwenye umri wa miaka 59 alikuwa waziri wa mafuta enzi za rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015. 
Aidha mwanamke huyo ambaye alikuwa wa kwanza kushika nafasi hiyo muhimu nchini Nigeria, ni miongoni mwa viongozi wa serikali iliyopita ambao wanatuhumiwa na serikali ya Rais Muhammadu Buhari kwa kuhusika na ufisadi mkubwa wa fedha za uma nchini humo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment