Image
Image

Bilal:Sekta binafsi za ndani na nje ya nchi zibuni mikakati ya kuongeza ajira nchini.


Makamu wa rais Dkt Mohamed Bilal amezitaka sekta binafsi za ndani na nje ya nchi kubuni mikakati ya kusaidia kuongeza ajira nchni ili kukabiliaba na changamoto ya ongezeko la vijana wasio na ajira wanatoka vijijini na kumbiliana mijini kwa lengo la kutafuta kazi.
Akizungumza katika mkutano wa wataalamu kutoka sekta binafis za ndani na nje ya nchni, na watendaji wa serikali unaolenga kuanzisha vituo vya kuzalisha na kuendeleza biashara, Dkt Bilali amesema serikali inapaswa kuajianda katika kuongeza ajira kufuatia tafiti za kimataifa kuonyesha ifikapo mwaka 2030 ongezeko la vijana mijini duniani litafitikia bilioni 5 kutokana bilioni 3 ya mwaka 2014.
Katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na teknolojia Bwana John Mngodo katika kukabiliana na tatizo la ajira nchni kufuatia serikali kutoweza kuajiri vijana wote wanaohitimu vyuo mbalimbali, serikali inataka sekta binafsi kuchukua nafasi kubwa ikiwemo kuanzisha hatamizi ambazo zitazalisha vijana watakaobuni biashara zitakazoongeza ajira kwa watanzania.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment