Watalaam wa utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya
wameonya kuwa mvua za El Nino zinatazamiwa kuanza kunyesha Jumatano wiki hii
katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Watu wanaoishi mabondeni na karibu na mito wameombwa
kuhama.
Maeneo yatakayoathiriwa zaidi ni Pwani, Magharibi mwa nchi hiyo na eneo la Bonde la Ufa.
Maeneo yatakayoathiriwa zaidi ni Pwani, Magharibi mwa nchi hiyo na eneo la Bonde la Ufa.
Kamishena wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa
amewataka watu wanaoishi katika mitaa iliyo mabondeni kuhama.
Mataifa yote ya Afrika Mashariki yanatarjiwa
kushuhudia mvua hizo zinayokadiriwa kudumu kwa miezi miwili na wito kama huo
umekuwa ukitolewa kwa wananchi wa nchi hizo kuwa makini.
Hayo ya kijiri, wanafunzi zaidi ya 500
wanaoshikiliwa katika makao makuu ya polisi mjini Eldoret nchini Kenya,
wanatazamiwa kupandishwa kizimbani baadaye Jumanne hii.
Polisi iliwakamata wanafunzi hao mwishoni mwa juma
kufuatia operesheni maalumu waliyoifanya usiku kwenye kumbi mbalimbali za
starehe mjini Eldoret, ambapo walikamatwa wakiwa na miraa, bangi, vilevi huku
mipira ya kiume (Condom) ikiwa imetapakaa kwenye ukumbi huo.
Polisi imesema waliwakamata wanafunzi hao baada ya
kupokea taarifa kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakitumia kumbi hizo kuvutia bangi,
miraa na kujihusisha na ngono.
Operesheni hii imefanyika ikiwa ni miezi 2 tu
imepita toka wanafunzi wengine 40 wakamatwe katika basi mjini Nyeri, wakitumia
dawa za kulevya na kujihusisha na ngono.
0 comments:
Post a Comment