Baraza la usimamizi wa mazingira NEMC limekifungia
kiwanda cha kutengeneza lami cha SKOL kilichopo salasala jijini Dar-es-Salaam
kutokana na kutokidhi viwango ikiwa pamoja nakutokuwa na kibali cha mazingira
pamoja na kutimua vumbi na kuathili wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho
mkuu wa ukaguzi na ufatiliaji NEMC Dr.Yoana Mtoni amesema pamoja na kukifungia
kiwanda hicho ambacho kilikiwa kinakiuka agizo la serikali mara kwa mara pia
kimetozwa faini zaidi ya shilingi milion hamsini ikiwa pamoja na kutoa amri ya
kuamisha mitambo yake eneo hilo ili kupisha wananchi waliozunguka kiwanda
hicho.
Kwa upande wao wananchi wanaoishi maeneo hayo
wameiomba serikali kuchukuwa hatua hasa kwa wawekezaji wanaokiuka utaratibu kwa
kuwa kiwanda huicho kilikuwa kikitimua vumbi jambo ambalo linalopelekea kupata
magonjwa mbalimbali mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment