Mwananchi akiwa kwenye harakati za kupiga kura(Picha na Maktaba).
Wasimamizi
wasaidizi wauchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu
wametakiwa kufuata kanuni na sheria pamoja na kutenda haki kama nguzo ya
amani katika shughuli hiyo.
Ushauri huuo umetolewa
na msimamizi mkuu wa jimbo la Magu Ntinika Paulo wakati akifunga mafuzo ya
siku mbili kwa wasimamizi wasaidizi wa jimbo la magu huku
akisisitiza kufanya kazi kwa uadilifu.
Akizungumzia mafunzo hayo mshiriki wa mafunzo
Mary Ng’wandu na Reuben Nkuba ambaye alitoa shukurani kwa niaba ya
wanamafunzo hayo alisema mafunzo hayo yamewasaidia kujua wanatakiwa kuwa watii
katika zoezi hilo na kuhakikisha wanakuwa hawana upendeleo wa aina
yoyote.
0 comments:
Post a Comment