Image
Image

Breaking News:Mh.Ndugai achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 11 Tz.

Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CCM na Mbunge wa kongwa mkoani Dodoma Mh.Job Ndugai ameshinda nafasi ya Uspika baada ya kuchaguliwa kwa wingi wa kura 254  na hivyo kuandika historia mpya katika Bunge la 11 la Tanzania Mjini Dodoma ya kuwa Spika akifuatiwa na Goodluck Ole Medeye kutoka CHADEMA kwa mwavuli wa UKAWA akipata kura 109 huku wengine wakiwa hawajapata kura
Baada ya kutangazwa mshindi kwa Bwana.Ndugai wagombea waliokuwa wakichuana nao wamempongeza pia na kusema kuwa watashirikiana naye kwa ukamifu mzuri katika kuipeleka mbele Tanzania.
Katika mchakato huo ambao ulikuwa umeshirikisha wagombea mbalimbali walioteuliwa na vyama vyao ulionekana kuwa na changamoto mbali mbali kwa kila mmoja kujinadi mbele ya wabunge wateule kuwa endapo wakipatiwa ridhaa ya kuwa Spika wa bunge bhasi watashughulikia changamoto mbalimbali zinazolalamikiwa juu ya uendeshaji wa Bunge na kuegemea upande mmoja.
Mh.Ndugai amekuwa moja ya watu ambao walishafanya kazi ya Bunge kwa kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo kwa miongo mitatu na hivi leo kuwa Spuka kamili wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa wingi wa kura.
Wagombea waliokuwa wameshiriki kwenye mchakato huo walikuwa 8 huku walio jinadi wakiwa saba na moja kati yao kutoka chama cha CHAUMA- Mh.Hasimu Rungwe kutoonekana Bungeni hapo bila taarifa rasmi.
    Waliokuwa teuliwa kuchuana kwenye nafasi hiyo ya uspika kutoka katika vyama vyao baada ya kupitishwa.-Peter Sarungi (AFP) -Hassan Kisabiya (N.R.A) -Dkt Godfrey Malisa(CCK) -Job Ndugai (CCM), -Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) -Richard Lymo (T.L.P) -Hashimu Rungwe(CHAUMA) -Robert Kisinini (DP).
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment