Image
Image

Kuharibika kwa mashine za MRI na CT-Scan zawa changamoto kwa wagonjwa Muhimbili.


Ikiwa ni siku moja tu mara baada ya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili kuotoa taarifa za kutokufanyaka na kuharibika kwa mashine ya MRI na CT-Scan changamoto zimeanza kujitokeza baada ya wagonjwa waliolazwa katika taasisi ya mifupa MOI wanaohitaji huduma hizo kukwama.

Moja ya kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 hadi 40 aliyelazwa chumba cha wagonjwa mahututi katika taasisi ya mifupa MOI baada ya kupata ajali eneo la ubungo na kujeruhiwa kichwani kuhitaji huduma hiyo ili hali bado ndugu zake hawajajitokeza amekumbwa na kadhia hiyo.

Taasisi ya mifupa MOI hutegemea baadhi ya vipimo ikiwemo MRI na CT-Scan Hospitali ya taifa Muhimbili ambapo Bw.Patrick amesema kwa sasa wagonjwa wao wenye uwezo wanakwenda kuvipata nje na kudai kuwa pindi watakapohamia jengo jipya wataondokana na kadhia hiyo.

Afisa habari wa moi Bw.Patrick Mvungi ametoa wito kwa mtu yeyote atakayemtambua afike katika taasisi hiyo ofisi ya uhusiano huku akieelezea namna msamaria mwema alivyomfikisha kijana huyo Hospitalini hapo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment