Waziri
mkuu wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza katika
bandari ya Dar es Salaam na kuona hali ilivyo katika utendaji kazi na hivyo kuagiza
waliohusika na upotevu wa makontena 349 kukamatwa mara moja.
Katika
ziara hiyo ya kushtukiza waziri mkuu huyo alitaka kujua namna ya kupokea mizigo
hapo bandarini na namna ambavyo mamlaka ya mapato Tanzania na mamlaka ya
bandari (TPA) namna wanavyoshirikiana kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa
kulingana na mizigo inawasili bandarini hapo.
Vile
vile alitaka kujua kwamba kwanini kunakuwepo na mwanya wa upotevu wa mapato na
pia kwanini baadhi ya wafanya biashara inadfaiwa kuwa wanatoa mizigo bandarini
bila ya kuli[pia ushuru ama bila kulipa kodi inayo stahili na kwa wakati,na pia
kutaka kujua ninani anayesababisha hali hiyo ya watu kutoa mizigo bandarini
bila kulipia kodi inayotakiwa.
Pia
Waziri Mkuu Majaliwa ambaye amekuwa na kiu ya kutaka kujua mambo kadhaa
bandarini hapo amesema na kwa kuhoji Mamlaka ya Bandari naTRA kuwa
wanahakikisha vipi kwamba mizigo inayo daiwa kwenda nje ya nchi inakuwa ni
mizigo inayo pita njia halali bila ujanja ujanja uaotumika kutokana na kuwa na
madai kuwa baadhi ya mizigo imekuwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi huwa
haifiki inaishia hapa hapa mjini na mwishowe kuuzwa.
0 comments:
Post a Comment