RAIS John Magufuli ambaye tangu
Novemba 17, mwaka huu alikuwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa majukumu
mbalimbali, amerejea Dar es Salaam jana na wakati wowote inaelezwa kwamba
anaweza kutangaza Baraza la Mawaziri linalosubiriwa kwa hamu na Watanzania.
Dk Magufuli alitua Ikulu ya
Chamwino, Novemba 17 kwa kutumia usafiri wa barabara akisafiri kwa zaidi ya
kilometa 300 kwenda katika Makao Makuu ya Serikali ambako kwanza alikuwa na
majukumu mawili makubwa.
Novemba 19, mwaka huu, alimteua
Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu na
siku iliyofuata alimwapisha katika Ikulu hiyo iliyoko takribani kilometa 40
kutoka Dodoma Mjini.
Aidha, baada ya kumwapisha Majaliwa asubuhi, jioni hiyo ya Novemba 20, Dk Magufuli aliyeingia madarakani Novemba 5, mwaka huu, alilihutubia na kulizindua Bunge la 11 mjini Dodoma katika hotuba iliyosisimua wabunge na Watanzania kwa ujumla kwa kugusa kero na mipango mbalimbali anayokusudia kuifanya.

Dk Magufuli alirejea Dar es Salaam
huku tetesi zikiimarika kwamba atatangaza baraza lake la mawaziri siku yoyote
kuanzia jana, na aliondoka Dodoma kwa ndege majira ya saa mbili asubuhi.
Kuwapo kwake kwa siku nyingi katika
kijiji cha Chamwino akifanya kazi, kulipongezwa na wanakijiji hao. Aidha,
wanazuoni na wanasiasa walitafsiri uwapo wake kijijini hapo kuwa ni kujichimbia
asibughudhiwe wakati akipanga baraza lake la mawaziri na mfumo wa uendeshaji
mpya wa baraza hilo.
Na ishara au dalili kwamba Baraza la
Mawaziri limeiva au litatangazwa wakati wowote ni hatua ya Dk Magufuli kutua
Dar es Salaam na baadaye mchana kwenda ofisini kwa Majaliwa ambako ni jirani na
Ikulu ya Magogoni.
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania,
Rais atateua Baraza la Mawaziri kwa kushauriana na Waziri Mkuu na Makamu wa
Rais, hivyo kuna kila dalili wawili hao kama sio wote watatu, wameshafanya kazi
hiyo.
Ofisi ya Waziri Mkuu ilithibitisha Dk Magufuli kutinga ofisini kwa Waziri Mkuu, Majaliwa na kufanya mazungumzo ya takribani saa moja.
Ofisi ya Waziri Mkuu ilithibitisha Dk Magufuli kutinga ofisini kwa Waziri Mkuu, Majaliwa na kufanya mazungumzo ya takribani saa moja.
“Rais aliingia ofisini kwa Waziri
Mkuu Majaliwa majira ya saa tisa na kulakiwa na mwenyeji wake na baadaye
walikaa kwa mazungumzo yao wawili tu.
“Baada ya mazungumzo hayo, Rais alizungumza kwa muda mfupi sana na makatibu Muhtasi wa Waziri Mkuu kabla ya kuondoka kuelekea Ikulu,” ilieleza taarifa fupi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
“Baada ya mazungumzo hayo, Rais alizungumza kwa muda mfupi sana na makatibu Muhtasi wa Waziri Mkuu kabla ya kuondoka kuelekea Ikulu,” ilieleza taarifa fupi ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mapema wiki hii, Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuwa Rais akishakamilisha kazi hiyo ya
kuteua Baraza la Mawaziri waandishi wa habari watajulishwa ili waupashe habari
umma wa Watanzania.
Akilihutubia Bunge na wakati akiwa
katika mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi Mkuu, Dk Magufuli aliahidi kuunda
Baraza la Mawaziri dogo ikiwa ni mojawapo ya njia za kudhibiti matumizi ya
serikali kwa nia ya kutafuta majawabu ya kero za wananchi kwa kasi
inayostahili.
Na hilo tayari limeonekana katika
hatua kadhaa ambazo amezichukua tangu aingie Ikulu. Alianza kwa kusitisha safari
za nje zisizo na umuhimu mkubwa, sherehe za Uhuru na kuzipa mwelekeo mwingine
kwa mwaka huu na pia kusitisha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi.
Katika kipindi kifupi cha uongozi
wake, maamuzi mazito kuhusu namna anavyotaka nchi iende yamefanyika ikiwa na kuhimiza
ukusanyaji wa kodi kwa kufanya ziara ya kushtukiza Hazina na pia Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili ambako alivunja Bodi kabla ya kutumia fedha za sherehe za
uzinduzi wa Bunge (mchapalo) kiasi cha Sh milioni 225 kutumika kuboresha hali
ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
0 comments:
Post a Comment