Tunapenda kuwawekea wazi Wazanzibari
wote kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote, ni za uzushi na wazipuuze.
Msimamo wa CUF na Maalim Seif Sharif
Hamad uko pale pale kwamba HAKUNA KURUDIWA UCHAGUZI na kwamba MSHINDI HALALI WA
UCHAGUZI WA TAREHE 25 OKTOBA, 2015 ATANGAZWE NA KUAPISHWA.
Kauli za Balozi Seif Ali Iddi ni za
kutapatapa zianzolenga kuwatuliza wana-CCM ambao wanaonekana kukata tamaa baada
ya kushindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.
Kwenye uchaguzi mkuu wa Urais wa
Zanzibar, mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alimbwaga vibaya mgombea wa
CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa zaidi ya kura 25,000.
Balozi Seif Ali Iddi mwenyewe akiwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM anatuhumiwa na wana-CCM kushindwa kazi
na kukisababishia chama chao kushindwa vibaya kuliko wakati wowote katika
historia ya chaguzi za Zanzibar.
Lakini kama hilo halitoshi, wana-CCM
wanamtuhumu Balozi Seif na wajumbe wengine wa Kamati ya Kampeni aliyokuwa
akiiongoza kusimamia matumizi mabaya ya kiasi kikubwa cha fedha za kampeni za
Chama hicho ambazo sehemu kubwa walimdanganya mgombea wao, Dk. Ali Mohamed
Shein, kwamba zimetumika kuleta ushindi wa CCM kisiwani Pemba lakini kumbe
ziliishia katika mifuko ya watu binafsi.
Haistaajabishi kwamba sasa Balozi
Seif Ali Iddi ameamua kuja na njia ya kutoa taarifa za udanganyifu ili
kujinusuru na mzigo wa tuhuma za kushindwa kazi na kusimamia matumizi mabaya ya
fedha za kampeni kutoka kwa CCM wenzake.
CUF tunamtaka Balozi Seif Ali Iddi
awache kudanganya umma na badala yake awajibu CCM wenzake kwa nini amekitia
chama hicho aibu na fedheha kubwa ya kupata kipigo kibaya katika uchaguzi
kilichopelekea CCM kupoteza majimbo tisa (9) kisiwani Unguja na Dk. Ali Mohamed
Shein kushindwa uchaguzi wa Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,000 huku
wakidai kutumia mamilioni ya fedha ambazo hawana maelezo zimetumika vipi.
CUF tunawataka Wazanzibari
kutobabaishwa na kauli za kushindwa kazi za Balozi Seif Ali Iddi na watulie
wakijua kuwa ufumbuzi wa haki wa uchaguzi mkuu utapatikana kwa kutangaza
matokeo ya kura kwa majimbo yaliyobakia na hatimaye mshindi kutangazwa na
kuapishwa.
0 comments:
Post a Comment