Hatimaye aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Kahama Mjini JAMES LEMBELI amefungua kesi katika mahakama kuu kanda ya Shinyanga kupinga matokeo ya kura za uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 ya mwezi uliopita.
Akizungumza baada ya kufungua kesi hiyo LEMBELI amezitaja sababu zilizomfanya yeye mwenyewe kupitia chama chake kufungua kesi ili kutetea kile alichodai haki ya wamanchi wa jimbo la Kahama Mjini.
Aidha wakili wake amesema yuko tayari kutetea na kuhakikisha mteja wake anashinda na kupata haki yake huku Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga ZACHARIA THOMAS akidai kuwa kama chama wanaungana na LEMBELI kudai haki na wanaamini haki itatendeka kwa mujibu wa sheria.
Mahakama inasubiriwa kutaja tarehe ya kuanza kesi hiyo.
Home
News
LEMBELI amefungua kesi katika mahakama kuu kanda ya Shinyanga kupinga matokeo ya kura za uchaguzi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment