Madereva wa magari katika Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kufuata taratibu za kisheria za usalama barabrani ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo baada ya kuonekana kuwepo ongezeko la ajali mkoani humo zinazo sababisha vifo mwaka huu ukilinganisha na mwaka uliopita.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa polisi wa mkoa huo Bwana MOHAMED SHEKHAN MOHAMED na Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Madereva mkoani humo Bwana ALI MOHAMED SHELA wakati wakizungumza katika mkutano wa pamoja kati ya jeshi la polisi, wizara ya mawasiliano na miundombinu na baraza la mji wa Chake Chake.
Katika mkutanio huo wadau wamesema ushirikiano unahitajika ili sekta ya usafirishaji mkoani humo iendelee kukuza uchumi badala ya kuwa chanzo cha kuudhofisha kutokana na vifo vinavyosababishwa na ajali za barabrani.
Aidha imebainika kuwa baadhi ya wamiliki wa magari wamekuwa wakifanya udanganyifu wa idadi ya tani katika shehena za mizigo ya malori yao au abaria wanaotakiwa kubeba.
Home
News
Madereva wa magari katika Mkoa wa Kusini Pemba wametakiwa kufuata taratibu za kisheria za usalama Barabrani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment