Rais Barack Obama wa Marekani ataonesha mshikamano na rais wa Ufaransa
Hollande katika ikulu ya Marekani leo siku 11 baada ya
kundi la Dola la Kiislamu kufanya mashambulizi kadhaa ya mauaji mjini
Paris.
Lakini Hollande huenda akaondoka Washington bila ya uungwaji mkono imara
kwa wito wake wa kuiingiza Urusi katika muungano mpya utakaopambana na
makundi yenye itikadi kali.
Ziara ya Hollande mjini Washington ni sehemu ya msukumo wa kidiplomasia
kuwezesha jumuiya ya kimataifa kuimarisha kampeni dhidi ya wanamgambo wa
kundi la Dola la Kiislamu.
Kundi hilo linaaminika kuhusika na mashambulio ya Novemba 13 ambayo
yamesababisha vifo vya watu 130 mjini Paris, pamoja na mashambulizi
mengine tofauti nchini Lebanon, na Uturuki na kuiangusha ndege ya abiria
ya Urusi nchini Misri.
Wakati kundi la itikadi kali la Dola la Kiislamu likipanua uwezo wake
nje ya eneo lake inalolidhibiti nchini Syria na Iraq , Obama anakabiliwa
na mbinyo mkali nyumbani na nje ya nchi hiyo kuongeza juhudi za nchi
hiyo kulivunja kundi hilo la wanamgambo.
Baada ya Paris Ufaransa yaongeza mashambulizi
Hadi sasa , Obama anasita kuitikia miito ya ama kubadilisha ama
kuimarisha msimamo wake, na badala yake analenga kuyaleta pamoja mataifa
mengine zaidi ili kupata taarifa nyingi zaidi za kijasusi za kupambana
na kundi hilo, na kupata usaidizi zaidi wa masuala ya kiutu na kijeshi.
Kampeni ya Marekani imelenga zaidi katika kushambulia, pamoja na mafunzo
na usaidizi kwa majeshi ya usalama ndani ya Iraq. Juhudi za kutoa
mafunzo na kuyapa silaha makundi ya waasi yenye msimamo wa wastani
nchini Syria hazijatosha, licha ya kwamba Obama aliidhinisha kuwekwa kwa
kikosi maalum cha wanajeshi 50 nchini humo ili kuanzisha mpango huo.
Ufaransa imeongeza mashambulizi yake ya anga nchini Syria , kufuatia
mashambulizi dhidi ya Paris, ikitegemea kwa sehemu fulani taarifa za
kijasusi za Marekani katika eneo la Raqqa, ngome kuu ya wanamgambo wa
Dola la Kiislamu nchini Syria. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
amesema jana kuwa atahitaji kupata ridhaa ya bunge la nchi hiyo wiki hii
ili Uingereza iweze kuanza mashambulizi ya anga pia.
Wakati huo huo Ubelgiji itaendelea kuwa katika kiwango cha juu cha
kitisho cha usalama kwa wingi nyingine kuhusiana na hofu ya shambulio la
kigaidi, imesema serikali ya Ubelgiji, wakati Marekani imetoa tahadhari
kwa Wamarekani wanaotaka kusafiri sehemu mbali mbali duniani.
Usalama katika viwanja vyetu vya ndege haukutengenezwa kumkamata mtu
wakati akipanda ndege. Umepangwa kuanza kuwakagua watu mara wanapoanza
kutafuta kukata tikiti.
Maafisa nchini Ubelgiji na Ufaransa wanafanya msako kumtafuta Salah
Abdeslam mzaliwa wa Ubelgiji , mshukiwa muhimu katika mashambulio ya
mjini Paris hapo Novemba 13, ambapo watu wenye silaha na mshambuliaji wa
kujitoa muhanga wameuwa watu 130.
Polisi ya Ufaransa leo imekuwa ikichunguza mkanda unaoshukiwa kuwa
unatumiwa na watu wanaojiripua sawa na ile iliyotumika katika
mashambulizi ya mjini Paris, kwa mujibu wa duru karibu na uchunguzi huo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment