ALIYEKUWA Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Edward Lowassa, amewataka wananchi kulinganisha ahadi za
Rais, Dk. John Magufuli na CCM kuhusu elimu.
Ameyasema hayo siku mbili baada ya Dk.Magufuli,aagize watendaji
wa serikali kushughulikia utekelezaji wa sera yake ya kutoa elimu bure
kuanzia Januari mwakani.
Lowassa, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
aliahidi kutoa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu.
Pia alikuwa ameahidi kufuta michango yote wanayotozwa wanafunzi, kama angepata ushindi wa kuwa rais.
Dk. Magufuli ambaye alikuwa akipeperusha bendera ya CCM, aliahidi kutoa elimu bure hadi kidato cha nne.
Taarifa iliyotolewa jana na ofisi binafsi ya Lowassa, ilisema ahadi
ya elimu bure aliyokuwa akiinadi, ilikuwa iwaguse hata wanafunzi ambao
tayari wako shuleni na siyo wanaotarajiwa kuanza mwakani pekee.
“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia
kindergarten (shule ya awali) hadi chuo Kikuu serikali yetu
ingegharimia.
“Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni kumpunguzia mzigo mwananchi,” taarifa hiyo ilimnukuu Lowassa akisema.
Taarifa hiyo ilisema ahadi ya Dk. Magufuli, “ni kwamba kuanzia
Januari hakuna mtoto atakayelipa ada lakini hajatamka mustakhabali wa
wanafuzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au laa.”
Kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, taarifa hiyo ilisema,
Chadema kupitia Lowassa kilikwisha kuahidi kuwa elimu ingekuwa bure hadi
chuo kikuu.
“Vijana hawa wanahangaika na mikopo nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment