Aidha, jumla ya watoto zaidi ya asilimia 48 hufariki dunia mara
baada ya kuzaliwa kuanzia siku moja hadi tano. Hayo yalibainishwa na
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Neema
Rusibamayila, wakati akizungumza na wananchi wa jijini Dar es Salaam
waliojitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya kununua mashine za kuhifadhia
watoto waliozaliwa kabla ya miezi tisa (njiti).
Mpango wa uchangiaji hiari wa mashine za kulelea watoto huo,
unaendeshwa na Taasisi ya Doreen Mollel, kwa lengo la kupata mashine 80
zitakazogawanywa katika kanda nane nchini ikiwa ni sehemu ya kupunguza
vifo hivyo.
“Kwa Tanzania, asilimia 80 ya watoto wanaozaliwa hupoteza maisha
kwa matatizo ya kuzaliwa njiti, matatizo ya uzazi na maambukizi ya
magonjwa mbalimbali kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,” alisema Dk.
Maile.
Aliwataka Watanzania kujitokeza kuchangia huduma hizo kwani kila
mmoja anajukumu hilo ili kumaliza vifo vinavyozuilika kwa kuhakikisha
hospitali zinakuwa na vifaa na huduma bora.
Naye Mkurugenzi wa Doreen Mollel Foundation, Miss Mollel, alisema
lengo la kuanzisha mfuko huo ni kuhakikisha watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati wanapata huduma bora ili waishi.
“Lengo letu ni kuhakikisha siku ya kuadhimisha mtoto njiti, Novemba
17, tuwe na mashine 10 katika kila kanda nchini ili watoto wanaozaliwa
wakiwa na hali hiyo wapate huduma,” alisema Mollel.
Pia alisema katika mchakato huo, wameweza kupata mashine nane hivyo bado wanauhitaji wa mashine nyingine 72 ili zitimie 80.
Alibainisha kuwa kila mashine moja inauzwa kiasi cha Sh. milioni
3.5, hivyo ili kupata mashine zote 80, zinahitajika Sh. milioni 280.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye alikuwa mgeni rasmi, Paul
Makonda (pichani), aliahidi kushirikisha viongozi mbalimbali wa serikali
akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ili achangie na kusaidia
watoto hao wenye uhitaji.
Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Chama cha Act-Wazalendo, Anna Mghwira, aliitaka jamii
na serikali kushiriki kikamilifu kusaidia watu wenye uhitaji kama watoto
hao.
Alisema sekta ya Afya inapaswa kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya
kutoa huduma bora hasa ya uzazi ambao ndiyo wenye changamoto kubwa ya
vifo.
0 comments:
Post a Comment