Mattaka na wenzake wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya
madaraka kwa kutangaza zabuni ya ununuzi wa magari 26 yaliyochakaa na
kuisababishia Serikali hasara ya Dola 143,442.75 za Marekani.
Aidha, mahakama hiyo imesema kesi hiyo itaanza kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi Desemba 10 na 11, mwaka huu.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emmilius
Mchauru, baada ya kusikiliza mashahidi 13 wa upande wa Jamhuri dhidi ya
washtakiwa.
Alisema washtakiwa hao wana haki ya kujitetea kupitia njia tatu.
“Washtakiwa mnaweza kuamua kujitetea kwa njia ya kiapo, bila kiapo
ama kukaa kimya kuiachia mahakama kutoa hukumu,” alisema Hakimu Mchauru
wakati akisoma uamuzi huo.
Hata hivyo, washtakiwa hao kwa nyakati tofauti walidai watajitetea kwa njia ya kiapo.
Upande wa utetezi ukiongozwa na Peter Swai na Alex Mgongolwa,
ulidai kuwa katika ushahidi wao wa utetezi, wanatarajia kuita mashahidi
saba wakiwamo washtakiwa.
Mbali na Mattaka, washtakiwa wengine ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo
cha Fedha, Elisaph Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William
Haji, wa shirika hilo.
Katika kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka, Mattaka na wenzake
Elisaph Ikomba na William Haji wanadaiwa pamoja na mambo mengine,
wakiwa waajiriwa wa ATCL na wenzao ambao hawajulikani kati ya Machi na
Julai, mwaka 2007, walikula njama ya matumizi mabaya ya madaraka na
kuisababishia Serikali hasara ya Dola 143,442.75 za Marekani.
0 comments:
Post a Comment