MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2014 (Miss Tanzania), Lilian Kamazima
anatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda Sanya, China kushiriki mashindano
ya dunia (Miss World), huku akiahidi kuipeperusha vyema bendera ya
Tanzania.
Alitoa ahadi hiyo jana mara baada ya kukabidhiwa bendera, ikiwa ni
ishara ya kuagwa tayari kwa safari ya kwenda China kushiriki katika
shindano hilo litakalofanyika Desemba 19, mwaka huu. Alikabidhiwa
bendera hiyo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
“Nakupongeza sana kupata nafasi hii na ninaamini kuwa umejiandaa
vizuri kushiriki mashindano haya na ukahakikishe unashinda mashindano
hayo na kuliletea sifa taifa lako,” alisema Mjema.
Aidha Mjema amemtaka mrembo huyo kuhakikisha anainadi vyema Tanzania
kwa kuvitangaza vivutio vyake vya utalii,hali ya siasa na amani iliyopo
nchini pamoja na lugha adhimu ya Kiswahili.
Alimtaka kutojisikia mnyonge kuizungumza lugha ya Kiswahili akiwa
kambini na wenzake na hiyo itawafanya watu wajue lugha hiyo na kuijua
vyema Tanzania. Kamazima aliahidi kwa kusema;
“Nimejiandaa vizuri na nina hakika nitafanya vyema ila nawaomba sana
Watanzania wenzangu mnipe sapoti yenu, kwani kuna ushiriki ambao nanyi
mnahusika ili kuniwezesha kushinda.” Mrembo wa Tanzania 2005 Nancy
Sumari alifanya vyema katika mashindano ya dunia na kutwaa taji la
Dunia, Kanda ya Afrika mwaka 2005.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment