Mahakama ya Tanzania imesema kuwa itendelea kufanya kazi na vyombo vya Habari nchini katika kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa jukumu la Kikatiba ililonalo la kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi ili kuwawezesha wananchi kujua na kupata Haki zao kwa wakati.
Akifunga
Mafunzo ya siku 2 ya waandishi wa Habari za Mahakama jana jijini Dar es
salaam Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila
aliwataka waandishi hao kutimiza wajibu wao wa kuueleza umma taarifa
sahihi za mashauri mbalimbali yanayotokea mahakamani kwa kuzingatia
sheria.
Alisema
vyombo vya habari na mahakama vinahitajiana, vinafanya kazi pamoja kwa
manufaa ya umma huku akieleza kuwa mikutano ya mara kwa mara kati ya
wanahabari na mahakama kunaongeza kuaminiana na kujenga mahusiano
mazuri.
Alifafanua
kuwa kazi ya Mahakama kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na
kuzitolea maamuzi kwa mujibu wa sheria kulingana na mashauri
yananayowasilishwa Mahakamani na kuongeza kuwa hakuna Jaji wa Mahakama
ya Tanzania anayeamua kesi bila nje ya utaratibu wa sheria zilizopo.
Alisema
wao kama majaji hutumia sheria zilizopo katika kutoa maamuzi hata kama
haziwapendezi wahusika na kuongeza kuwa jambo wanalolifanya ni kutoa
maoni na mapendekezo kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
"
Sisi kama Majaji hutumia sheria zilizopo kutoa maamuzi,hatutungi sheria
jukumu letu kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea
maamuzi pia tunatumia fursa ya maamuzi tunayoyatoa kuelimisha jamii
kuhusu sheria iliyotumika kutoa haki katika kesi husika" Alisema.
Aliwataka
waandishi wa Habari za Mahakama kujipa muda wa kutosha pindi wanapofika
Mahakamani kufuatilia mashauri yanayoendeshwa ili waweze kuwa na
taarifa za kutosha pindi shauri linapofunguliwa na kutolewa hukumu ili
kuwawezesha wananchi kupata taarifa za kutosha za mwenendo wa Mashauri.
Aliongeza
kuwa Mahakama ya Tanzania imedhamiria kufanya kazi na waandishi wa
habari nchini kwa kuzingatia kwamba wakati majaji wanapotoa hukumu
mahakamani kunakuwa na idadi ndogo ya wananchi wanaoshuhudia kuliko ile
iliyo nje ila vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake huwapasha
habari mamilioni ya watanzania walio nje ya Mahakama.
Alisema
Mahakama itaendelea kujenga mahusiano mazuri na Vyombo vya Habari
hususan waandishi wa Habari za Mahakama kwa kutenga maeneo ndani ya
Mahakama yatakayotumiwa na waandishi hao kuwawezesha kufanya kazi zao
bila vikwazo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Pia
alieleza kuwa Mahakama, itaendelea kutoa taarifa za ufafanuzi wa hukumu
mbalimbali zitakazotolewa kwa vyombo vya habari pia Nakala za taarifa
za Hukumu kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha wananchi kujua ukweli
wa yale yanayojili mahakamani kuondoa upotoshaji unaotokea.
Aidha
alisema kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana na Baraza la Habari
Tanzania (MCT) katika kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa
habari za Mahakama ili waweze kuandika habari zenye ukweli na uhakika.
Mhe.
Shaban Lila alisema kuwa Mahakama iko tayari kupokea maoni yanayohusu
utendaji kazi wake ili iweze kuyafanyia kazi kwa manufaa ya vyombo vya
habari na wananchi.
Awali
akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha Jaji
Kiongozi kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama
ya Tanzania Bi. Wanyenda Kuta aliwaambia washiriki wa mafunzo hayo kuwa
Mahakama inaendelea kutekeleza nguzo 3 ambazo ni kuhakikisha kuwa
kunakuwa na Upatikanaji wa Haki kwa Wakati, Kuongeza Imani wanachi kwa
Mahakama pia kuboresha miundombinu ya Mahakama nchini.
Alisema
kuwa wandishi wa Habari za mahakama waliohudhuria mafunzo hayo
yaliyoandalia na Mahakama ya Tanzania na Baraza la Habari Tanzania (MCT)
wamejifunza masuala mbalimbali ambayo yamewajengea ufahamu waandishi wa
Habari za Mahakama kuhusu lugha za kimahakama, uandishi bora wa habari
za Mahakama, Uhuru wa Mahakama pamoja na kujua Haki za Washitakiwa na
Watuhumiwa wanapofikishwa mahakamani.
Kwa
upande wake Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan
Lawa akizungumza na wanahabari hao aliwataka waandike habari za
Mahakama kwa usahihi na umakini mkubwa kufuatia Mafunzo
waliyoyapata.
Bw.
Lawa aliishukuru Mahakama mafunzo hayo na hatua ya uongozi wa mahakama
kuyakubali mapendekezo yaliyotolewa na Waandishi wa Habari za Mahakama
ikiwemo kutenga eneo ndani ya mahakama litakalotumiwa na waandishi wa
Habari za Mahakama, utoaji wa Nakala za kesi na ufafanuzi wake mara
hukumu zinapotolewa, Mahakama kukubali kushawishi uanzishaji wa madawati
ya Habari za Mahakama kwenye vyombo vya Habari pamoja na mahakama
kukubali kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa Habari za
Mahakama na wahariri wao.
0 comments:
Post a Comment