Imeelezwa kuwa ili kuleta ufanisi mzuri kazini,waajiri na
waajiriwa wanatakiwa kutekeleza kisheria yale yote wanayokubaliana katika
utendaji wao wa kazi.
Akizungumza na Tambarare Halisi Afisa Mwandamizi wa kazi na
Ajira mkoa wa Morogoro JULIUS NKUNGA amesema ili kazi iweze kufanyika kwa
ufanisi mzuri ,kwa haki na uhuru ni lazima waajiri na waajiriwa wote kufuata
kikamilifu sheria zinazowapasa.
NKUNGA ameongeza kuwa kuna baadhi ya changamoto
wanazokumbana nazo ambazo ni pamoja na uhaba wa fedha na ikizingatiwa katika kitengo
chao wanatakiwa kutoa huduma kwa wilaya sita hivyo wanaiomba serikali
kuliangalia vyema suala hili hasa katika utengwaji wa bajeti.
Aidha NKUNGA amesema katika kitengo kinachojishughulisha na
kusimamia sheria za kazi kwa ujumla wanajitahidi kutoa elimu kwa waajiri na
waajiriwa katika kuhakikisha kila mmoja anazifuata sheria na hatimaye kuwa
na utendaji mzuri wa kazi.
Hata hivyoElimu hizo hutolewa kwa njia ya semina na warsha
mbalimbali baada ya kuwepo kwa malalamiko yanayohusiana na matatizo waliyoyapokea
ya waajiri na waajiriwa ili kutoa ufumbuzi .
0 comments:
Post a Comment