MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, inaangalia mwelekeo
wa kumpa dhamana mwanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT),
Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, amelishwa sumu.
Hayo yalidaiwa jana mahakamani hapo, wakati kesi
hiyo ilipokuwa ikitajwa na upande wa Jamhuri na kudai kuwa upelelezi
haujakamilika.
Hakimu Mkazi Respicius Mwijage,aliahirisha kesi
hiyo hadi Novemba 10, mwaka huu kwa ajili ya kuangalia mwelekeo wa kumpa
dhamana mshtakiwa.
Wakili wa Serikali Mwandamkizi, Shadrack Kimaro,
aliwasilisha mahakamani hati kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akidai
kwa mamlaka aliyonayo amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa mshtakiwa kwa
sababu kuna mambo ya taifa anayoyashughulikia.
Hakimu Mwijage, awali alikubali kumnyima dhamana
mshtakiwa, lakini baada ya siku 14 alihoji akitaka Jamhuri itoe sababu za
kuendelea kuwapo kwa zuio hilo.
Kutokana na kutokuwapo sababu za msingi, mahakama
hiyo iliahirisha kesi hadi siku iliyopangwa kwa ajili ya kuangalia mwelekeo wa
kumpa dhamana mwanafunzi huyo.
Awali upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Kimaro kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Johannes Kalungura, Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Theophil Mutakyawa, Jackline Nyantori na Anastazia Wilson,
walimsomea mshtakiwa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Mwijage.
Kimaro alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo, Septemba
25, mwaka huu, Dar es Salaam, ambapo alisambaza taarifa kupitia mtandao wa
Facebook, kwamba Jenerali Mwamunyange amelishwa sumu.
0 comments:
Post a Comment