WATU wawili wamefariki dunia na wengine zaidi ya 120 wamelazwa katika
vituo vya kutolea huduma ya kwanza katika wilaya tano za Mkoa wa Dodoma
kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Afya wa
Mkoa wa Dodoma, Edward Ganja alisema watu wawili wamefariki dunia
kutokana na ugonjwa huo katika Wilaya ya Kongwa.
Ugonjwa wa kipindupindu umeripotiwa kuingia mkoani hapa tangu
Septemba mwaka huu katika wilaya za Kongwa, Chamwino, Bahi, Manispaa ya
Dodoma na Chemba.
Ganja alisema wagonjwa 120 walilazwa na kutibiwa katika wilaya hizo,
ingawa sasa amebaki mmoja ambaye amelazwa hospitali ya mkoa.
Alisema kuwa Wilaya ya Bahi ilikuwa na wagonjwa 78 ambao wametibiwa
na kupona, Chamwino 12, Chemba wawili na Kongwa 35 mbali na wawili
waliofariki dunia.
Pamoja na hali hiyo, Ganja alisema uongozi wa mkoa umechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
“Pia tumekuwa tukitoa elimu kupitia Serikali za vijiji na kamati za afya kwa kufanya ukaguzi nyumba hadi nyumba.
“Kamati hizo zina mamlaka ya kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula
shuleni na pombe za kienyeji ambazo ni chanzo cha kupata vijidudu vya
ugonjwa huo,” alisema Ganja.
Aliwataka wakazi wa Dodoma kuhakikisha wananawa mikono kabla na baada
ya kula, kula vyakula vya moto na kuzingatia kanuni za usafi ili
kuepuka ugonjwa huo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment