Image
Image

Ripoti ya TEMCO yaonesha mapungufu katika uchaguzi mkuu Tanzania.


Taasisi ya uangalizi wa uchaguzi Tanzania TEMCO imetoa ripoti yake kuhusu uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni na kubainisha mapungufu yaliyojitokeza pamoja na mafanikio yaliyofikiwa ikilinganishwa na uchaguzi mkuu uliopita.
Naibu mwenyekiti wa TEMCO Dk Benson Bana akisoma taarifa ya awali ya kuhusu uchaguzi mkuu amesema uligubikwa na matukio mengi ya kisiasa ikiwemo mgawanyiko wa wazi wa wapiga kura na wanasiasa juu ya katiba inayopendekezwa, kushindwa kutekelezwa kwa makubaliano ya kuboresha uwazi na haki ikiwemo kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi pamoja na uwezekano wa kupinga matokeo ya kura za urais mahakamani.
Kuhusu uchaguzi wa Zanzibar amesema TEMCO ilishtushwa na uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi uliotangazwa na mwenyekiti wa ZEC kwani taarifa za awali za waangalizi wake zilionyesha kuwa shughuli zote za uchaguzi zilifanyika kwa weledi na kwa misingi ya sheria huku akitoa maoni yao juu ya mgogoro huo.
Akihitimisha ripoti hiyo Dk Bana amesema TEMCO imetoa mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa uchaguzi ili kuboresha chaguzi za Tanzania ikiwemo kurekebisha na kupitia upya sheria ya uchaguzi ili kuruhusu mgombea binafsi, kuruhusu watanzania wanaoishi nje ya nchi kupiga kura kuangalia upya uteuzi wa makamishna na mkurugenzi wa uchaguzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment