JESHI la Polisi limesema limeimarisha ulinzi kesho wakati wa kuapishwa Rais mteule wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli.
Sherehe za kuapishwa Dk. Mgufuli zitafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa
kuhudhuria.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna wa
Oparesheni Maalumu wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alisema ni
marufuku kwa wananchi kushiriki katika maandamano yaliyoandaliwa bila
kufuata taratibu za nchi.
“Tunawashukuru wananchi na vyombo vya habari kwa sababu kwa pamoja
tulishirikiana katika kipindi cha uchaguzi ambacho kilikuwa ni cha vuta
nikuvute na tumeweza kuilinda amani yetu hadi hii leo.
“Hatimaye kesho tunatarajia kuapishwa kwa rais mteule, Dk. Magufuli,
nawasihi wote kwa pamoja tuendelee na moyo huo huo wa kulinda amani
yetu.
“Tusishiriki kabisa maandamano batili kwa sababu yanaweza
kusababisha uvunjifu wa amani na jeshi hatutasita kuwachukulia hatua
watu watakaokaidi agizo hili,” alisema.
Aliwataka wananchi na waandishi wa habari kutoa ushirikiano wakati wa
kuapishwa kwa Dk. Magufuli kwa kutoa taarifa iwapo watabaini kuwapo
viashiria vya uvunjifu wa amani kama walivyofanya katika kipindi cha
kampeni na uchaguzi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa,” alisema.
Akizungumzia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) yaliyotarajiwa kufanyika jana, alisema polisi walilazimika
kuyazuia kwa vile yalikosa sifa kutokana na maombi kuwasilishwa nje ya
muda unaotakiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment