WAZIRI Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi
ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi
kutokana na majukumu ya ofisi hiyo yanayogusa maisha ya kila siku ya
Watanzania.
“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli
za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi
matarajio yao,” alisema Majaliwa. Alitoa kauli hiyo jana mchana wakati
akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini
Dar es Salaam.
Jana ndiyo aliripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa
iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. “Pamoja na kazi
nyingine, tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na
ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu serikalini.
Ninatarajia kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila
taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za
Tamisemi ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.
Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa
Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais John Magufuli ili kumudu
kasi ya utendaji kazi Serikalini ambayo anahimiza hivi sasa. Alisema ana
imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa
wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi
karibuni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment