Mali imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa
kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika kutokana na
kuzingirwa hoteli ya kifarahari, yaliyowaua watu 19 kwenye mji mkuu,
Bamako.
Mataifa mengine ya jirani kama Senegal, Mauritania na Guinea zinaungana na taifa hilo kuonyesha mshikamano.
Uchunguzi wa kuwasaka waliohusika na mkasa huo bado unaendelea ambapo
mpaka sasa hakuna utambuzi wa idadi wala utaifa wa wanaotuhumiwa kufanya
shambulizi hilo ambalo limegharimu maisha ya watu 19, ambalo vilevile
makundi mawili ya jihadi yamekiri kuhusika nalo.
Siku ya umwagikaji damu
Katika mkasa huo uliotokea Ijumaa watu waliokuwa na silaha waliizingira
hoteli ya ya kifahari ya Radisson Blu, na kuwateka wafanyakazi na wageni
wa hoteli 170. Shambulizi hilo lilifikia kikomo baada ya jeshi la Mali
na vikosi vya kimataifa walishambulia jengo hilo, ambapo watu 19
waliuwawa, wakiwemo raia wa kigeni 14.
Waliouwawa katika mkasa huo ni pamoja na Warusi sita, Wachina watatu,
Wabelgiji wawili, Mmarekani mmoja, Muisrael mmoja, Msenegali na idadi
nyingine ya wanajeshi wa Mali.
Rais ya Senegal atoa pole.
Rais wa Senegal, Macky Sall, jana Jumapili alitembelea mji wa Bamako
kuonyesha mshikamano kwa Mali, mwanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi
za Afrika Magharibi-ECOWAS, ambayo kiongozi huyo ni mwenyekiti. Sall
alisema Mali haitakuwa mpweke katika mapambano hayo, kwa sababu wote
wanahusika.
Katika hatua nyingine jana Jumapili, wachunguzi nchini Mali inafuatilia
kwa kina vyanzo mbalimbali vya uchunguzi wao kufuatia mauwaji hayo. Siku
mbili baada ya mkasa huo ambao makundi ya Al Mourabitoun na al-Qaeda
katika katika eneo la Afrika Magharibi yamedai kuhusika, kumekuwa na
utambuzi duni wa waliofanya shambulizi.
Katika taarifa yake kitengo cha usalama wa taifa nchini Mali
kimenukuliwa na katika televisheni ya nchi hiyo kikisema maeneo kadhaa
yamekuwa yakifuatiliwa. Na kwamba hoteli iliyokuwa imeshambuliwa imekuwa
ikifuatiliwa kwa uangalifu mkubwa.
Kwa kuzingatia siku ya operesheni ya kukabiliana na ugaidi katika hoteli
hiyo Rais Ibrahim Bouba Keita alisema wote kwa pamoja wauwaji
walifanikiwa kuuwawa katika eneo la hotel ingawa kulikuwa na taarifa
nyingine za awali zilizosema kulikuwepo na mshambuliaji mwengine.
Ufaransa, ambalo lilikuwa lilikuwa likiitawala Mali katika enzi za
ukoloni, linasaidia katika jitihada za sasa za uchunguzi na kwamba
imetuma timu ya wataalamu katika kufanikisha jambo hilo.
Umwagikaji damu mjini Bamako ni miongoni mwa ishara za hivi karibuni
kabisa kw kuzorota zaidi kwa hali ya usalama katika taifa hilo la Afrika
Magharibi. Wanamgambo wenye itikadi kali wenye kuungana na al-Qaeda
walilidhibiti eneo la jangwa la kaskazini 2012 lakini mwaka mmoja baadae
walitawanywa na operesheni ya kijeshi ya Ufaransa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment