Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja
tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa. Rais ameahidi
kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni.
Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni,
Rais Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara
mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri
kutekeleza majukumu yao bora zaidi.
Idara hizo zimeongezwa kutoka 26 hadi 41.
Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza lake
la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa kutokana na wizara
walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati yao wakikabiliwa na kesi
mahakamani.
Ni mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada ya hatua ya
aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni mwa juma kutokana
na kile alichosema ni ushauri wa daktari wake- baada ya usumbufu aliopata
wizara yake ilipohusishwa na sakata kadhaa za ufisadi.
Kwa mujibu wa katiba idadi ya mawaziri inapaswa kuwa
kati ya 14 na 22 na hivyo kujiuzulu kwa Bi Waiguru kulisababisha idadi hiyo
kupungua hadi 13.
Baraza jipya la mawaziri linajumuisha wanawake wanne
na wanaume 16.
Baadhi ya mawaziri wamesalia katika nafasi zao huku
wengine wapya wakiteuliwa kuchukua nafasi za mawaziri waliohusishwa na ufisadi.
Hatua itakayofuata sasa ni kwa mawaziri wapya
kuchunguzwa na kamati ya bunge kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imekuwa ikikabiliwa
na changamo ya ufisadi katika wizara kadhaa na kumekuwepo shinikizo sio tu
kutoka kwa wananchi lakini pia kutoka kwa mashirika ya kijamii,viongozi wa
upinzani na hata mabalozi wa nchi za kigeni kutaka hatua zichukuliwe
0 comments:
Post a Comment