Urusi inasema kuwa afisa huyo yuko katika hali njema
katika kambi ya kijeshi ya Lattakia.
Wizara ya ulinzi nchini Urusi inasema kuwa rubani
mwingine na mwanajeshi aliyeshiriki katika operesheni ya kwenda kuwaokoa
marubani hao wa ndege iliyodunguliwa nao waliuawa.
Ubalozi wa Urusi na taarifa kutoka kwa serikali ya
Syria zinasema kuwa rubani huyo aliokolewa na wanajeshi wa Syria na anarudishwa
kwenye kambi ya jeshi la urusi eneo la Lattakia huko Syria.
Moscow inasema kuwa operesheni nchini Syria
zitaendelea kuwakabili wapiganaji wa Islamic State na makundi mengine ya
kijihadi.
Aidha Urusi imesema kuanzia leo ndege zinazoelekea
kutekeleza operesheni za mashambulizi dhidi ya makundi ya kijihadi zitapewa
ulinzi mkali na ndege za kivita.
Vilevile mitambo ya rada ya Urusi itatumika
kuimarisha ulinzi wa angani katika maeneo ya mipakanai ya Syria.
Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama
amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake
inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.
Hakikisho hilo la rais Obama linafwatia hatua ya
Uturuki kuidungua ndege ya Urusi karibu na mpaka wa Syria.
Umoja wa mataifa na muungano wa kujihami ya nchi za
Maghraibu NATO wamewataka Urusi na Uturuki kutuliza hasira zao.
0 comments:
Post a Comment