Urusi imeonya kuwa italipiza kisasi kufuatia
kuangushwa kwa ndege yake.
Waziri mkuu wa Urusi , Dmitriy Medvedev, amesema
kuwa Uturuki inawalinda Islamic State .
Medvedev amedai kuwa Uturuki inahofia kupoteza
kipato kikubwa inachofaidika kutokana na wizi wa mafuta kutoka Syria.
Aidha, Medvedev amedai kuwa mikataba yote na Uturuki
imesimamishwa na kuwa kampuni zote zenye asili ya Uturuki zimepigwa marufuku
nchini Urusi.
Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama
amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake
inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.
Hakikisho hilo la rais Obama linafwatia hatua ya
Uturuki kuidungua ndege ya Urusi karibu na mpaka wa Syria.
Mataifa yote duniani yalihofia kutibuka kwa vita
iwapo Moscow ingelipiza kisasi kufuatia mauaji ya askari wake katika shambulizi
hilo.
Ikulu ya WhiteHouse ilisema kuwa wakati wa
mazungumzo kwa njia ya simu kati ya marais hao wawili kuwa wote walikubaliana
kutuliza hali hiyo.
Umoja wa mataifa na muungano wa kujihami ya nchi za
Maghraibu NATO wamewataka Urusi na Uturuki kutuliza hasira zao.
Akizungumza baada ya mkutano wa dharura wa mataifa
ya NATO ulioitishwa na Uturuki, katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema
tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika
anga ya Uturuki.
Huku kukiwa na hali ya wasiwasi, Stoltenberge
ametaka kuwepo na hali ya utulivu kutoka pande zote.
Amesema taarifa walizozipokea kutoka nchi washirika,
zinaenda sambamba na maelezo ya Uturuki ya tukio hilo.
"Ushirikiano tulioupata kutoka kwa washirika
mbalimbali kwa leo unathibitisha taarifa tuliyoipata kutoka Uturuki."
Hata hivyo, Moscow bado wanasisitiza kwamba, ndege
hiyo ilikuwa katika anga ya Syria, na kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa anga ya
Uturuki.
0 comments:
Post a Comment