Serikali imesema kuwa itahakikisha dawa katika Mahospitali na
Vituo vya afya zinapatikana kwa wakati kama ambavyo ahadi ya Rais Dkt.
Magufuli aliyokuwa akiitoa katika kampeni zake, sasa ni hatua ya
utekelezaji wa ahadi hii kwa wananchi.
Katika
kulitekeleza hilo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa
Bwanakunu aliagizwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Donan Mmbando
kwa niaba ya Rais, kuhakikisha kuwa dawa zote za Serikali zinakuwa na
utambulisho maalum ili endapo zikikutwa zipo katika maduka ya dawa
binafsi, basi hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wamiliki wa
maduka hayo.
Ikumbukwe,
MSD inahudumia hospitali za Serikali tu na vituo vyake na kamwe dawa
ambazo husambazwa na MSD hazipaswi kuuzwa kwa wamiliki wa maduka ya dawa
binafsi, Hivyo ni kosa la jinai kwa dawa za Serikali kukutwa kwa
wamiliki wa maduka ya dawa binafsi. Ameeleza Mkurugenzi wa MSD.
Aidha,
Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa, MSD itafungua maduka ya dawa makubwa
karibu na mahospitali ya Serikali ili kurahisisha zaidi upatikanaji wa
madawa kwa urahisi ikiwa ni kusambaza madawa hayo kote nchini katika
vituo vya afya kwa wakati, ili wananchi wote wenye uhitaji wa madawa
waweze kupata bila tabu yoyote ile.
Kwa
kuhitimisha, Mkurugenzi huyo ametoa namba maalum na itabandikwa kwenye
vituo vya afya na mahospitali yote ya serikali kwa dhumuni moja la
msingi ambalo ni endapo mwananchi yeyote atapata tabu katika kupatiwa
dawa, basi atumie namba hiyo kutoa taarifa MSD na kupiga ni BURE kabisa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment