Jaji mkuu wa Tanzania Othuman Chande
amewataka waandishi wa habari nchini hasa za mahakama kutokuingilia utendaji
haki badala yake wazingatie sheria, kanuni na maadili ya kazi za Mahakamani.
Jaji Chande ameyasema hayo jijini
Dar es Salaam ambapo amesema haki ya waandishi wa habari kuwa na maoni
inathaminiwa na kutambulika lakini wanawajibika kwa sheria ya kashifa na
kudharau mahakama hivyo ni vyema wakachukua tahadhari mapema ili kuepuka
kukumbana na sheria hizo.
Kwa upande wake meneja maadili wa baraza la habari Tanzania
MCT Allan Nlawa amesema mahakama kuu kwa kushirikiana na MCT wameamua kutoa
elimu ya nmana ya kutoa taarifa za mahakamani ili kuepuka kuandika habari
zitakazoingilia utendaji wa mahakama na kutolea mfano wa baadhi ya vichwa vya
habari ambavyo wakati mwingine vinasababisha utata kwenye mwenendo mzima wa
kesi, shahidi amgaragaza mshitakiwa.
0 comments:
Post a Comment