Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Lauren Bwanakunu, fedha hizo
zinapaswa kulipwa na Hazina kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza na Tambarare Halisi liiyotaka kujua kuhusiana na deni
hilo, Bwanakunu alisema kutokana na deni hilo MSD imeshindwa kuwalipa
wazabuni wake wanaowapelekea dawa ambao wamegoma kuendelea kutoa huduma
hiyo hadi pale watakapolipwa fedha zao.
Alisema pia wazabuni wengine wanaowategemea kuwapelekea dawa
wamesimamisha huduma kutokana na mikataba waliyokuwa nayo kumalizika.
“Hali hii imesababisha MSD kushindwa kukidhi manunuzi ya dawa kama
yalivyo matarajio ya mwaka huu wa fedha, jitihada zinaendelea hata hivyo
tunaweza kupata fedha kidogo ndani ya muda mfupi kulingana na uwezo wa
serikali na sisi tuweze kuwalipa wazabuni kuwapa imani,” alisema.
Bwanakunu alisema kwa taratibu za MSD, kila hospitali, zahanati au
kituo cha afya huagiza dawa mara nne kwa mwaka, yaani kila baada ya
miezi mitatu. Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Donald Mbando, alisema hadi sasa serikali imeshalipa deni
inalodaiwa na MSD Sh. bilioni 42 katika mwaka wa fedha uliopita.
Alisema serikali ipo katika mikakati ya kulipunguza zaidi kwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha katika mwaka wa fedha 2015/16.
Hata hivyo, alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) alifanya uhakiki wa deni hilo na kutaja deni kamili kuwa ni Sh.
bilioni 54 na kwamba serikali italipa deni hilo kwa kufuata taratibu na
taarifa ya CAG na siyo kiasi cha deni kinachoelezwa na MSD kuwa ni Sh.
bilioni 114.
Taarifa zilizowahi kuthibitishwa na aliyewahi kuwa Waziri wa Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Seleman Rashid wakati wa kikao cha Kamati
ya Bunge ya Huduma za Jamii mwaka jana na kuripotiwa na gazeti hili
zilionyesha kuwa MSD inaidai serikali Sh. bilioni 102.
Alieleza kuwa baada ya MSD kuona kuwa madeni yanazidi kulimbikizwa
huku kasi ya serikali ikiwa ndogo katika kulipa, iliamua kusitisha
huduma zake kwa serikali, lengo likiwa ni kushinikiza walipwe fedha hizo
ili waendelee kutekeleza majukumu yao kama yalivyoanishwa katika Sheria
Namba 3 ya kuanzishwa kwake mwaka 1993.
0 comments:
Post a Comment