Alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa,akizungumzia viongozi wa kisiasa na umuhimu wa kulinda amani na
umoja wa kitaifa kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wa Zanzibar.
Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeleta mafanikio makubwa kwa
watu wa Zanzibar kisiasa na kiuchumi na kufanikiwa kupunguza siasa za
chuki na ubaguzi zilizokua zimewekwa na wakoloni kwa madhumuni ya
kuwagawa ili kuwatawala.
“Maisha bora kwa wakulima wa zao la karafuu yameanza kuonekana
baada ya serikali ya pamoja kufanikiwa kuinua bei ya zao hilo katika
kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein,”
alisema na kuongeza:
“Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeleta utulivu kwa miaka mitano yote ilipokua inafanyakazi.”
Amir ambaye pia ni Katibu Jumuiya ya Sanaa na Utamaduni Zanzibar,
alisema kutokana na kumalizika kwa siasa za chuki na uhasama Zanzibar,
milango ya kiuchumi imefunguka kwa wawekezaji wa kigeni na wazalendo
kuanza kuwekeza katika sekta za viwanda na huduma za tiba visiwani humo.
“Nawasihi viongozi wetu wa kisiasa wasiweke sana maslahi binafsi
mbele ya kupata nyadhifa kubwa serikalini, tuweke mbele maslahi ya
taifa na wananchi, huko ndiko kupevuka kisiasa, tujengee vizazi vijavyo
nchi bora na yenye utulivu wa kudumu,” alisema.
Hata hivyo, Amir alisema ili malengo hayo yaweze kufikiwa, wakati
umefika kwa viongozi wa kisiasa kujenga uvumilivu wa kisiasa ikiwamo
kutupilia mbali siasa chuki na historia.
“Nyinyi viongozi wetu, akiwa ni Dk. Ali Mohamed Shein, Maalim Seif
Sharif Hamad, Balozi Seif Iddi tunawaomba mkutane tena ili mwendeleze
Serikali ya Umoja wa Kitaifa inatufaa Wazanzibari, msichoke kwani
jinamizi la ukoloni lipo nyuma, wekeni mgawo wa madaraka ili pande zote
ziridhike muongoze Zanzibar kwenye maendeleo na matumaini makubwa kwa
wananchi wake,” aliongeza kusema katika waraka wake huo wa kurasa sita
kwa vyombo vya habari.
Zanzibar imeingia katika mgogoro wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa
visiwa hivyo kwa kile alichoeleza kugubikwa na kasoro nyingi ikiwamo
udanganyifu.
0 comments:
Post a Comment