RAIS
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa
4,160 katika kuaga na kukabidhi madaraka ya Serikali kwa Rais wa Awamu ya Tano,
Dk John Magufuli.
Dk
Magufuli aliapishwa jana kuwa Rais wa Tano wa Tanzania katika sherehe
zilizofana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Kikwete akimaliza miaka
yake 10 ya kuongoza nchi kama ilivyoelekezwa na Katiba.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
kwa vyombo vya habari Dar es Salaam, kati ya wafungwa hao,wafungwa 867
wataachiwa huru na wafungwa 3,293 watapunguziwa vifungo vyao na kubaki gerezani
wakitumikia sehemu ya vifungo vyao vilivyobaki.
“Ni
mategemeo ya Serikali kwamba wafungwa watakaoachiwa huru watarejea katika jamii
kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa na watajiepusha na
utendaji makosa ili wasirejee tena gerezani,” alisema Chikawe katika taarifa
hiyo.
Chikawe
aliwataja walionufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wote wapunguziwe moja ya
sita ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya Kifungu cha
49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa
katika ibara ya 1 (i-xix).
Aliwataja
wengine kuwa ni wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama Ukimwi, kifua kikuu,
saratani ambao wako kwenye hatua ya mwisho ambao watathibitishwa na waganga
chini ya Mganga mkuu wa mkoa au wilaya.
Pia
wazee wenye umri zaidi ya miaka 70, wafungwa wa kike walioingia na mimba
gerezani na walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya na walemavu wa
mwili na akili na ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga.
Kwa
mujibu wa Chikawe, msamaha hautawahusu wafungwa wenye adhabu za kunyongwa,
waliohukumiwa kunyongwa na adhabu hiyo baadaye kubadilishwa kuwa kifungo cha
maishaau kifungo gerezani.
Wengine
ni wafungwa waliotumikia kifungo kwa makosa ya usafirishaji na utumiaji wa dawa
za kulevya, makosa yanayohusu uombaji, upokeaji na utoaji rushwa, unyang’anyi
na kujaribu kutenda makosa hayo, kubaka, kulawiti au kujaribu kutenda makosa
hayo.
Aidha, makosa
mengine ambayo vifungo vyake haviko kwenye msamaha huo ni makosa ya kuwapa
mimba wanafunzi, wizi wa magari, pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo,
matumizi mabaya ya madaraka, waliowahi kupunguziwa vifungo na Rais.
“Wengine
ni waliopatikana na hatia kwa kuwazuia watoto kupata masomo, utekaji watoto,
usafirishaji binadamu, ukatili dhidi ya albino, usafirishaji nyara za Serikali
na ujangili,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Mengine
ni wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi na ubadhirifu wa fedha za Serikali,
kutoroka au kujaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi halali na wafungwa
wanaotumikia vifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole Sheria Namba 25 ya Mwaka
1994 ya Sheria ya Huduma kwa Jamii Namba 6 ya Mwaka 2002.
0 comments:
Post a Comment