Tegete,
baba wa mshambuliaji mahiri wa Mwadui ya Shinyanga, Jerson Tegete alisema Toto
Africans ni timu iliyodhamiria kuonesha ushindani mkubwa kwenye Ligi Kuu msimu
huu na kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo.
“Tulifungwa
na Yanga lakini sisi sio kivuli cha Yanga, walituzidi kimchezo na zaidi Yanga
walishinda kwao, watakuja kwetu Mwanza, mtaona kitakachotokea,” alisema Tegete.
Alisema
dhamira yao ya kuonesha ushindani mkali kwenye Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania
Bara ilianza tangu ligi hiyo ilipofunguliwa rasmi na kwamba watalionesha hilo
kwa vitendo kwa kipindi chote cha msimu.
“Mkoa
wetu unastahili kuwa na timu ya ushindani kwani ni moja ya mikoa mikubwa hapa
nchini na hata katika soka pia ni mkoa mkubwa, tutawafurahisha watu wa Mwanza
kwa kuonesha ushindani,” alisema Tegete.
0 comments:
Post a Comment