Mchezo
huo wa kirafiki ni sehemu ya progamu ya Kocha Mkuu, Charles Boniface baada ya
kufanya mazoezi na vijana wake kwa takribani siku nne mpaka sasa, anahitaji
kuona maendeleo ya kikosi chake kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo dhidi ya
‘Mbweha wa Jangwani’ Algeria.
Stars
iliyowasili Johannesburg Jumatatu mchana, imekuwa ikifanya mazoezi yake asubuhi
na jioni katika viwanja vya St. Peters College na kituo cha michezo cha
Edenvale.
Kuhusu
hali ya kambi, Boniface alishukuru maendeleo ni mazuri vijana wake wote wapo
katika hali nzuri hakuna majeruhi na wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo
utakaofanyika Novemba 1 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
"Dhumuni
la kuweka kambi huku ni kupata nafasi ya kuwaanda vijana kwa mazoezi katika
mazingira mazuri ikiwamo viwanja vya mazoezi, chakula na malazi kinachofanya
kuongezeka kwa umakini katika mazoezi," alisema kocha huyo.
Wachezaji
26 waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Aishi Manula na Said Mohamed,
walinzi ni Shomari Kapombe, Juma Abdul, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Mwinyi
Haji, Hassan Isihaka, Salim Mbonde, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub
“Cannavaro”.
Wengine
ni viungo Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Said Ndemla,
Jonas Mkude, Salum Telela, Farid Musa na Simon Msuva, ambapo washambuliaji ni
Malimi Busungu, Elias Maguri, John Bocco na Mrisho Ngasa.
Wachezaji
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wanatarajiwa kuungana na kikosi cha Stars baada
ya mchezo wao wa fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi ya USM Algiers.
0 comments:
Post a Comment