Hali ya ugonjwa wa Kipindupindu Jijini Dar es Salaam bado si nzuri, ambapo katika kambi ya Mburahati,idadi ya wagonjwa bado inazidi kuongezeka siku hadi siku, licha ya elimu inayotolewa juu ya ugonjwa huo.
Afisa Muuguzi wa kambi hiyo, AMINA MBWESO amesema idadi ya wagonjwa inaongezeka na kupungua kila siku na hakuna siku ambayo hawapokei wagonjwa wa Kipindupindu usiku na mchana.
AfisaMuuguzi huyo amesema kwa sasa wana wagonjwa 25 ambao bado wanaendelea kupatiwa huduma ya matibabu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment