Image
Image

Saa 48 za Maalim Seif zaanza kuonesha Mwanga Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kimesitisha ajenda yao ya kurejesha kwa wananchi mpango wa kupinga uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, kufuta matokeo ya uchaguzi baada ya juhudi za kidiplomasia kuonyesha muelekeo wa kupata ufumbuzi.
Akiongeza na Waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia ndiye Mgombea Urais wa chama hicho Visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad amesema juhudi sasa zimeanza kuonekana katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo.
Maalim Seif amesema Juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya ya Kimataifa katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo ikiwemo umoja wa Mataifa zinaonyesha muelekeo mzuri na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati huu.
Hata hivyo Maalim Seif amesema kuwa kuna kikundi cha Watu wachache ambacho kimekua kikwazo kutokana na kutetea maslahi binafsi katika kutafuta muafaka wa mgogoro huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment