Utafiti uliofanywa kwa niaba ya serikali ya Kenya na wahadhiri wa
chuo kikuu cha Moi kilichoko katika Bonde la ufa umebaini kuwa Majani ya
miraa inayofahamika pia kama 'Mairungi' unazuia ukuaji wa manii.
Aidha ulaji wa kipindi kirefu wa miraa unafanya mbegu za kiume za wanaume kufa haraka pindi zinapowekwa kwenye uke.
Mtafiti
mkuu wa chuo kikuu cha Moi, Ochiba Lukanda, anasema kuwa utafiti sawa
na huo uliofanywa huko ghuba ulibaini matokeo kama hayo.
Lukanda
anasema kuwa wanaume ambao wamekuwa wakila Miraa kwa kipindi kirefu na
wakaacha huwa wanapata uwezo wao wa kutunga mimba.
Ulaji wa Miraa pia huwa unasababisha mshtuko wa moyo.
''Mtu
anapokula mmea huu baada ya muda damu yake huaanza kwenda kwa kasi,
mbali na shinikizo la damu mumea huu hausababishi saratani kama
inavyodaiwa '' Dakta Lukanda
Hata hivyo utafiti katika maeneo yanayokuzwa mumea huu umetambua kuwa
idadi ya vijana wanaokataa kwenda shule kwa sababu ya kujishughulisha
na uchumaji wa Miraa na upakiaji wa matawi yake.
''kutokana na
utashi wa bidhaa hiyo,malipo ya wafanyikazi wanaoishughulikia ni ya juu
mno kwa hivyo inawavutia vijana kuacha masomo alisema daktari huyo.
Daktari Lukoye Atwoli alisema kuwa miraa husababisha walaji wake kuwa na mori na hata wakati mwengine msongo wa mawazo.
Utafiti huu unafwatia ule uliofanywa mwaka uliopita na wataalamu kutoka
chuo kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Konstanz cha
Germany na kile cha Minnesota, Marekani uliobaini kuwa ulaji wa miraa
unaathiri ubongo wa walaji wake na kusababisha msongo wa
mawazo,mafadhaiko na mahangaiko ya kiakili mbali na matatizo mengine
chungu nzima.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment