Image
Image

Viongozi wa Serikali wapewa mwezi mmoja kuhakiki watoto wenye sifa waanze shule mara moja.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Hajat MWANTUM MAHIZA  amewapa mwezi mmoja viongozi wa ngazi zote za serikali wilayani Handeni kuhakiksha kuwa watoto wote wenye sifa za kuanza darasa la kwanza, hasa wa wafugaji wanapelekwa shule.
Akizungumza na wakazi wa vijiji vitatu vya kata ya Misima katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Msomera wilayani humo ameonya kuwa serikali itawachukulia hatua za kisheria viongozi wasiosimamia utekelezaji wa agizo hilo ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.
Amesema wafugaji wengi wanakaidi agizo a serikali la kuwapeleka watoto wao shule na viongozi wa eneo husika wanashindwa kuchukua hatua kitendo ambacho ni cha kuwakosesha haki yao ya msingi kizazi hicho.
Kwa upande wao baadhi ya wafugaji wa vijiji hivyo wamesema hawakatai kuwapelekea watoto wao shule bali mila na desturi zao zinataka watoto wafundishwe kuchunga kwa sababu wazazi wanabakia katika zoezi la kulea familia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment