Tukio la kuuaga mwili wa marehemu
Alphonce Mawazo katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza limetanguliwa na ibada
iliyoongozwa na mchungaji Bernard Swai wa kanisa la Winners.
Fredrick Sumaye, waziri mkuu
mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa
chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA
), Mh. Edward Lowassa wakatoa angalizo kwa jeshi la Polisi nchini kuhakikisha
linatenda haki katika kushughulikia kifo cha marehemu Alphonce Mawazo.
Mwenyekiti wa taifa wa Chadema Mh.
Freeman Mbowe naye akatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Alphonce Mawazo,
aliyeuawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana Novemba 14
mwaka huu katika kijiji cha Katoro wilayani Geita.
Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo
tayari umewasili mjini Geita ambako utalala usiku huu ili kutoa nafasi kwa
wananchi wa mkoa huo kutoa heshima zao za mwisho siku ya jumapili asubuhi Novemba
29, kabla ya kupelekwa nyumbani kwao katika kijiji cha Chikobe kwa ajili ya
mazishi yatakayofanyika siku ya jumatatu Novemba 30.
Mtoto wa marehemu Alphonce Mawazo,Precious Mawazo mwenye umri wa miaka tisa akatokea mbele ya halaiki kuelezea majonzi ya kufiwa na baba yake.
Mtoto wa marehemu Alphonce Mawazo,Precious Mawazo mwenye umri wa miaka tisa akatokea mbele ya halaiki kuelezea majonzi ya kufiwa na baba yake.
0 comments:
Post a Comment