Shirika la kutoa misaada la Rural Development Centre, limeripoti kuwa wahudumu hao walitekwa nyara Mashariki mwa Congo.
RDC inasema kuwa watu hao waliokuwa wakitokea eneo la Rutshuru wakati walitekwa na wapiganaji waliokuwa wamejihami kwa bunduki katika mji wa mdogo wa Katwiguru.
Afisa wa shirika hilo la RDC , Paul Muhasa, aliliambia shirika la habari la AFP.
Mji huo wa Katwiguru upo takriban kilomita 120 Kaskazini Mashariki mwa Goma.
Shirika hilo la kutoa misaada linasema maafisa wake walikuwa wamekwenda kutathmini hali ya lishe na athari ya ukosefu wa lishe bora kwa jamii walipotekwa nyara.
Shirika hilo huwa linamradi wa kuifunza jamii kwa ushirikiano na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) Rutshuru.
Afisa anayeisimamia eneo la Rutshuru,Liberata Burotwa amenukuliwa akisema kuwa anaishuku kundi la wanamgambo wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) kwa kutekeleza utekaji huo.
Makundi ya waasi wa kabila la ki-Hutu kutoka Rwanda wanalaumiwa kwa utovu wa usalama mashariki ya Congo na eneo zima la maziwa makuu.
Hata hivyo hakuna uthibitisho kamili kuwa kundi hilo la FDLR ndilo lililowateka wafanyikazi hao wa mashirika ya kutoa misaada kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment